Contact: | Email: bwawanisecondary@prisons.go.tz

About Us


Historia Fupi

Shule inamilikiwa na JESHI LA MAGEREZA na ilianzishwa mwaka 1978 ikiitwa Ubena Sekondari ili kutoa elimu ya Sekondari kwa Askari wa Gereza la Mifugo Ubena ambalo lilikuwa maalum kwa wafungwa waliokuwa Watumishi wa Serikali ambao kiwango chao cha elimu kilikuwa cha juu ukilinganisha na Askari wengi wa kituo hicho. Kilianza kama kituo cha maandalizi ili kufanya mtihani wa kidato cha nne.

Mwaka 1981 Shule ilianza kupokea wanafunzi wa maeneo ya jirani na Shule. Shule ilisajiliwa kwa namba P.170 ikaanza kupokea Askari wa vituo vyote vya Magereza walioajiriwa wakiwa na elimu ya darasa la saba. Lengo lilikuwa kuwapatia elimu ya Sekondari kama matakwa ya mfumo wa ajira Serikalini kuwa lazima kila mtumishi awe na elimu ya Sekondari. Mwaka 2000 Shule ilisajiliwa na kupata namba S.1264 na kuitwa Bwawani Sekondari na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la saba toka kwa wanajamii wote wa Kitanzania wakiwemo jamii za kiaskari na kiraia. Ni shule ya bweni na kutwa kwa wanafunzi wa kike na kiume.

Mmiliki Wa Shule

Kamishna Jenerali Wa Jeshi la Magereza (CGP)

na Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara

Jeremiah Yoram Katungu-ndc na Mmiliki wa Shule